MALENGO
Vipaumbele na mipango Parokia
Maono
Tunapomaliza ujenzi wa kanisa, Parokia yetu itakuwa mojawapo ya sehemu kuu za hija kwa Mama Bikira Maria nchini Tanzania na nchi jirani. Tunatarajia pia kuwa kitovu cha elimu, afya na uwekezaji, kwa manufaa ya waamini na jamii inayotuzunguka.
Vipaumbele
Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli – Bunju imekua kila mwaka ikitekeleza vipaumbele saba (7) vya kudumu katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Parokia. Kutokana na mahitaji ya kila mwaka, kadiri inavyoonekana inafaa, Parokia imekua ikiongeza vipaumbele vingine vya muda katika vipaumbele vya kudumu vilivyopo na kuvitekeleza sambamba na vipaumbele vya kudumu.
a) Kuandaa hija, mafungo, semina na mafundisho mbalimbali ya kiimani (ikiwemo semina kuhusu matoleo mbalimbali ikiwemo Zaka, sadaka, shukrani, malimbuko nk).
b) Kuweka mikakati ya kuongeza mahudhurio katika sala za jumuiya na kanda.
c) Kuweka mikakati ya kuondoa uchumba sugu.
d) Kuimarisha mafundisho ya Imani katoliki (Wakatekumeni, Ekaristi Takatifu, Kipaimara, Ndoa Takatifu nk). Hii ni pamoja na kutoa elimu ya dini katika shule zilizopo jirani na Parokia.
e) Kufanya maadhimisho ya kumbukumbu za upadrisho kwa mapadri wetu.
f) Kufanya maadhimisho ya sikukuu na kumbukumbu mbalimbali za Parokia yetu.
g) Wajumbe wa Kamati Tendaji na Kamati mbalimbali za Parokia kufanya ziara katika kanda za Parokia kwa ajili ya kufanya uinjilishaji.
h) Kuandaa Misa mbalimbali; mfano Misa Takatifu za shukrani, uponyaji kupitia Ekaristi Takatifu nk.
i) Kuhakikisha kuwa Parokia ina vitendea kazi muhimu kwa ajili ya shughuli za utume kwa mapadri, nk.
j) Kuanzisha vyama mbalimbali vya kitume katika Parokia.
k) Kufanya matendo mbalimbali ya upendo na huruma ndani na nje ya Parokia kwa kushirikiana na Vyama vya Kitume katika Parokia.
l) Kudumisha ujirani mwema na majirani, makanisa na taasisi zilizo jirani na Parokia yetu.
m) Kufanya uinjilishaji kwa Parokia zingine ili kusaidia katika kukuza Imani Katoliki katika maeneo mengine

a) Kuendelea kusali na kuombea ujenzi wa kanisa la Parokia.
b) Kuendelea kufanya uinjilishaji wa utoaji wa zaka kamili ikiwa ni chanzo kikuu cha matoleo kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Parokia.
c) Kutoa taarifa za ujenzi wa kanisa kila mwezi ikijumuisha taarifa za ufundi, fedha na uinjilishaji.
d) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kanisa na kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kama ilivyopangwa.

a) Kufanya uchaguzi wa viongozi katika ngazi mbalimbali za jumuiya na kanda kadiri kutakavyokua na mapengo katika nafasi za uongozi.
b) Kuhakikisha kuwa Kamati Tendaji ya Halmashauri ya walei Parokia inakutana walau mara moja kila mwezi.
c) Kuhakikisha kuwa vikao vya Halmashauri ya walei Parokia vinafanyika kila baada ya miezi mitatu (3).
d) Kufuatilia utendaji wa shughuli za vyama vya kitume vyenye hadhi ya Parokia, Kamati Tendaji za Kanda na kamati mbalimbali za Parokia.
e) Kuandaa semina za viongozi ili kuimarisha uongozi wa jumuiya, kanda, vyama vya kitume na Parokia.
f) Kuandaa taarifa za utekelezaji za kila robo mwaka kwa kanda na vyama vya kitume ngazi ya Parokia.
g) Kuhakikisha kuwa jumuiya na kanda zinatekeleza miongozo mbalimbali iliyotolewa na Parokia, mfano mwongozo wa utunzaji fedha katika jumuiya, kanda na vyama vya kitume, mwongozo wa uendeshaji na usimamizi wa sala za jumuiya nk.
h) Kuhakikisha kuwa kamati zinazohitajika kikatiba zinaundwa katika jumuiya na Kanda. Pia kamati za hiari kama kamati ya Utunzaji Mazingira nk.
i) Kuhakikisha kuwa jumuiya, kanda na vyama vya kitume ngazi za Parokia zina akaunti za benki kama inavyoelekezwa na mwongozo wa Utunzaji fedha katika jumuiya, kanda na vyama vya kitume. Sehemu kubwa ya jumuiya, kanda na vyama vya kitume ngazi za Parokia wametekeleza hili.

a) Kuboresha mfumo wa Zaka Kamili ili uweze kutoa huduma bora zaidi. Ikiwemo kufanya marejeo (‘’review’’) ya kila mwaka ya bidhaa na huduma za mfumo wa zaka kwa kushirikiana na mtoa huduma – Sadaka Digital.
b) Kuendelea kufanya uinjilishaji wa utoaji wa zaka kamili ikiwa ni chanzo kikuu cha matoleo kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Parokia.
c) Kufanya vikao vya mashauriano kila baada ya miezi mitatu baina ya kamati ya zaka parokia na Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia.
d) Kufanya mafungo kwa wanakamati wa Kamati za Zaka Kamili walau mara moja kila mwaka.

(Hasa kutafuta maeneo ya ardhi)
Lengo:
1. Ili ardhi hizo zije zitumike kwa ajili ya kufanya miradi mbalimbali ya Parokia ili kusaidia katika kuwa vyanzo mbadala vya fedha kwa Parokia.
2. Ili kupata maeneo ya ziada kwa ajili ya Parokia – mfano ununuzi wa maeneo kwa ajili ya vigango vipya vya Parokia yetu.

a) Kufanya semina mbalimbali za uchumi na ujasiriamali kwa wanaparokia.
b) Kupitia Kamati za Mipango, Uchumi na Fedha za Kanda, kuhakikisha kuwa kila kanda inafanya uhamasishaji ili wanakanda waweze kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.
c) Kusimamia ‘’Dawati la Ushauri wa Mambo ya Kibiashara na Ujasiriamali" lilipo chini ya Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha ya Parokia. Dawati hili lina majukumu yafuatayo:
(i) Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanaparokia wajasiriamali ya mada za kuendesha semina za ujasiriamali katika Parokia yetu.
(ii) Kupokea mahitaji binafsi ya ushauri (maarifa na stadi) kutoka kwa wanaparokia wajasiriamali na kusaidia katika suluhisho la mahitaji hayo - kupitia ndani ya wajumbe wa Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha au kwa wanaparokia wengine kadiri itakavyoonekana inafaa.

Kipaumbele cha utunzaji wa mazingira kitaendelea kupewa umuhimu mkubwa katika Parokia yetu kwa kuhakikisha kuwa masuala yafuatayo yanatekelezwa:
a) Kuhakikisha kuwa kuanzia ngazi ya jumuiya, kanda na Parokia zinaundwa Kamati za Utunzaji wa Mazingira.
b) Kuhakikisha kuwa kila kanda inatenga mojawapo ya jumamosi ya tatu (3) au ya nne (4) ya mwezi katika kila robo mwaka kuwa ni siku ya usafi na utunzaji wa mazingira.
c) Katika utekelezaji wa mkakati wa usafi na utunzaji wa mazingira, masuala yafuatayo inabidi yazingatiwe;
• Upandaji wa miti katika maeneo ya Parokia yetu, makazi ya waamini, sehemu za kupumzikia nk.
• Kuweka mikakati ya matumizi mazuri ya maji (kuzuia upotevu wa maji) na uvunaji wa maji ya mvua.
• Kuweka suala la utunzaji wa mazingira katika mafunzo ya katekesi kwa komunio ya kwanza na kipaimara.
• Upandaji wa miti katika eneo la Parokia wakati wa ziara za Askofu au Askofu Mkuu.
• Utoaji wa Elimu ya utunzaji wa mazingira katika jumuiya, kanda na Parokia kwa ujumla.