Parokia ya Bikira Maria
Wa Mlima Karmeli - Bunju
Parokia ya Bikira Maria
Wa Mlima Karmeli - Bunju
Padri Dominic Somola O.Carm
Neno la Baba Paroko
Ndugu zangu wapendwa katika Kristo,
Kwa furaha kubwa ninawakaribisha katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli – Bunju
Parokia yetu imejengwa juu ya safari ndefu ya imani, sala, majitoleo, upendo na mshikamano wa waamini ambao, kizazi baada ya kizazi, wameendelea kujitoa katika kulijenga Kanisa kiroho na kimwili.
Nawakaribisha wanaparokia wote, wageni na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kuwa sehemu ya safari hii. Tushirikiane katika sala, utume, huduma na majitoleo ili Parokia yetu iendelee kuwa mahali pa Imani, Faraja na Matumaini.
Chini ya ulinzi wa Mama Bikira Maria wa Mlima Karmeli, tuendelee kusali, kufanya kazi kwa bidii na kujitoa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na ustawi wa Kanisa lake.
Karibuni sana Parokiani.
Kutoa huduma za sala, hija na uinjilishaji wa Neno la Mungu.
Kutoa huduma za kiroho na kimwili, kiuchumi na kijamii na kuendeleza ustawi wa waamini ili waishi maisha ya kumpendeza Mungu na kuufikia wokovu wa milele.
Maadili Yetu
- Maisha ya kumpenda Mungu
- Maisha ya sala
- Maisha ya majitoleo
- Maisha ya upendo na unyenyekevu
Kuhusu Parokia Yetu
Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli ni jumuiya ya waamini inayojengwa katika misingi ya sala, upendo, majitoleo, unyenyekevu na huduma.
Parokia ilitangazwa rasmi tarehe 24 Agosti 2012 na +Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, wakati huo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa Misa Takatifu ya Upadrisho wa Padri Dominic Somola O.Carm. Parokia ilizaliwa kutoka katika Kigango cha Mt. Joseph – Bunju, ambacho awali kilikuwa chini ya Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja – Boko.
Mahali Tulipo
Parokia yetu ipo katika Dekania ya Bunju, Jimbo Katoliki la Bagamoyo, lililozinduliwa rasmi tarehe 4 Mei 2025. Parokia ipo Bunju “A”, Kinondoni, Dar es Salaam, pembezoni mwa Barabara ya Bagamoyo.
Matangazo, Habari & Matukio.
Karibu usome matangazo, habari na matukio muhimu yanayohusu parokia yetu na jamii kwa ujumla..







